Ingawa kunaweza kuwa na mabadiliko kuhusu jinsi huduma zinavyotolewa katika baadhi ya maeneo, wafanyakazi wetu waliojitolea na wenye ujuzi wa hali ya juu wa afya ya akili wako hapa ili ku kuhudumia.
Kipaumbele chetu ni afya na usalama wa jamii yetu. Ni muhimu kwa mtu yeyote anayepata shida ya afya ya akili au wasiwasi wakati wowote kufikia msaada na utunzaji. Tafadhali usichelewe - usaidizi unapatikana ikiwa unauhitaji.
Ikiwa mtu amejaribu, au yuko katika hatari ya mara moja ya kujaribu kujidhuru mwenyewe au mtu mwingine, piga Sifuri Tatu (000)
Ikiwa huzungumzi Kiingereza, bado unaweza kupata usaidizi wa dharura kwa njia ya simu 24/7, kupitia kwa 131 450.
Ikiwa mtu ana shida ya afya ya akili, au una wasiwasi kuhusu afya yako au ya mtu mwingine ya akili:
Iwapo wewe au mtu unayemjua anahitaji usaidizi wa jumla wa afya ya akili, tumia kitafuta huduma za afya ya akili cha ºÚÁϳԹÏÍø Health ili kupata utunzaji unaofaa, au zungumza na daktari wako wa familia kuhusu usaidizi mwingine unaopatikana.
Usaidizi wa simu pia unapatikana kupitia:
Kwa ushauri wa afya ya jumla bila malipo wakati wowote mchana au usiku, piga healthdirect kwa 1800 022 222. Muuguzi aliyesajiliwa anaweza kukupa ushauri wa afya na ku kuunganisha na huduma unayohitaji. Translating and Interpreting Services (Huduma za Kutafsiri na Ukalimani) wanapatikana kwa nambari 131 450. Kwa habari zaidi tembelea Healthcare popote pale. ​
​â¶Ä‹