Kipimo cha Ngozi cha Kifua Kikuu (TST au kipimo cha Mantoux) ni kipimo kuona ikiwa mtu ana maambukizo ya TB Kifua Kikuu.​​
Maambukizo ya TB (pia yanajulikana kama maambukizo ya TB yanayofichika ama ugonjwa wa TB 'unaolala') yapo unapopata vijidudu vya TB katika mwili wako, lakini havifanyi uwe mgonjwa. Mfumo wako wa kinga wa mwili unazuia vijidudu kusababisha uharibifu wowote. Hakuna dalili za maambukizi ya TB na vijidudu haviwezi kusambaza kwa watu wengine.
Maambukizi ya TB ni tofauti na ugonjwa wa TB ambao upo wakati vijidudu vya TB vinapoamka au kuzidi kwa idadi zao na kusababisha uwe mgonjwa na kuweza kusambaza vijidudu kwa watu wengine. ​​Ikiwa TST inaonyesha una maambukizo ya TB, daktari wako anaweza kuagiza dawa ili kuzuia ugonjwa wa TB.
Habari zaidi kuhusu maambukizo ya TB zinapatikana hapa: Maambukizo ya TB​
TST inahusisha kudungwa sindano ndogo ya tuberculin (yenye protini iliyosafishwa) kwenye mkono. Baada ya siku chache, alama nyekundu au uvimbe unaweza kuonekana, au kunaweza kuwa hakuna mabadiliko yoyote. Muuguzi maalum wa TB anahitaji kuangalia mahali ambapo sindano ilipigwa saa 48-72 baada ya kipimo kile.
Kuna hali kadhaa za afya na dawa ambazo zinaweza kuathiri matokeo yako ya kipimo. Umjulishe muuguzi wako au daktari ikiwa wewe:
Hakikisha eneo lililopigwa sindano linaangaliwa na muuguzi au daktari mtaalamu muda wa saa 48 hadi 72 baada ya TST kufanyika ili athari yoyote inaweza kutathminiwa na kurekodiwa. Ikiwa TST ni chanya, unaweza kuhitaji vipimo vya kufuatilia. Muuguzi wako au daktari ataeleza matokeo na kama vipimo vyovyote zaidi vinahitajika au matibabu.
Ili kupata maelezo zaidi tembelea Karatasi za ukweli za Kifua Kikuu (TB)​.
Kupata usaidizi bila malipo katika lugha yako, piga simu kwa Huduma ya Utafsiri na Wakalimani kwa 13 14 50.​