Tiba ya Kuzuia Kifua Kikuu

Maambukizo ya kifua kikuu (TB) ni nini?

Maambukizo ya TB (pia yanajulikana kama maambukizo ya TB yanayofichika ama ugonjwa wa TB 'unaolala') yapo unapopata vijidudu vya TB katika mwili wako, lakini havifanyi uwe mgonjwa. Mfumo wako wa kinga wa mwili unazuia vijidudu kusababisha uharibifu wowote. Hakuna dalili za maambukizi ya TB na vijidudu haviwezi kusambaza kwa watu wengine.

Maambukizi ya TB ni tofauti na ugonjwa wa TB ambao upo wakati vijidudu vya TB vinaamka au kuzidi kwa idadi zao na kusababisha uwe mgonjwa na kuweza kusambaza vijidudu kwa watu wengine.

Tiba ya Kazuia ya Kifua Kikuu (TPT) ni nini?

TPT ni antibiotiki maalum kwa maambukizo ya TB. Kuna aina tofauti za antibiotiki - daktari wako ataamua ni ipi iliyo bora kwako. Urefu wa muda unaohitaji kutumiwa ni tofauti kwa kila mtu, lakini hutumiwa kwa miezi kadhaa. ºÚÁϳԹÏÍø Afya hutolewa TPT bila malipo bila kujali hali ya visa au Medicare.

Je, TPT itazuia kabisa ugonjwa wa TB?

TPT inaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa TB kwa 90% ikiwa unatumia dawa zote ambazo daktari wako anaagiza. Bado inawezekana kuambukizwa tena na vijidudu vya TB. Hii inaweza kutokea ikiwa unasafiri kwa nchi yenye TB nyingi au upo karibu na mtu wenye TB. Hakuna njia ya kupimwa ili kuangalia ikiwa tiba imefanya kazi yake. Njia pekee kujua ni ya kutumia dawa zote zinavyoagizwa na daktari wako.

Je, kwa nini nitumie TPT wakati sijisikii mgonjwa?

TPT ni njia bora ya kujizuia dhidi ya ugonjwa wa TB. Ikiwa daktari amependekeza TPT, ni kwa sababu upo hatarini kupata ugonjwa wa TB. TPT huzuia vijidudu vya TB kufanya uwe mgonjwa kabla ya unakuwa mgonjwa. Hukuzuia kutokuwa mgonjwa na kusambaza ugonjwa kwa familia yako na jumuiya yako.

Je, dawa itafanya niwe mgonjwa?

Madhara ya TPT siyo kawaida. Unaweza kuulizwa kupata kipimo cha damu kuangalia kama kila kitu ni sawa. Daktari na muuguzi atazungumza nawe kuhusu madhara yanayowezekana kabla ya kuanza tiba yoyote.

Habari zaidi

Ili kupata maelezo zaidi tembelea Karatasi za ukweli za Kifua Kikuu (TB)​. 

Kupata usaidizi bila malipo katika lugha yako, piga simu kwa Huduma ya Utafsiri na Wakalimani kwa 13 14 50.

Current as at: Friday 4 April 2025
Contact page owner: Communicable Diseases